Vipengele
Dhima ya Ansible itasakinisha, usanidi na uendeshaji wa proksi inayojitegemea ya Snowflake.
- Support for Ubuntu, Debian, Arch Linux, Fedora and FreeBSD.
- Kitengo cha Systemd cha kudhibiti huduma ya Snowflake kwenye GNU/Linux na hati ya rc ya FreeBSD.
Mahitaji
- Python
- Ansible 2.9 au juu zaidi
1. Sakinisha Ansible
Unaweza kusakinisha Ansible ukitumia pip:
$ python -m pip install --user ansible
Au tafuta njia zingine ili kusakinisha Ansible.
2. Pakua jukumu la Ansible
Dhima ya Ansible inaitwa nvjacobo.snowflake.
Unaweza kuipata ndani ya Hazina ya Galaxy na usakinishe kwa kutumia mstari wa amri:
$ ansible-galaxy install nvjacobo.snowflake
3. Unda kitabu cha kucheza
Kufuatilia, unda playbook ya Ansible ili kuendesha dhima mpya:
- hosts: snowflake
roles:
- nvjacobo.snowflake
4. Unda orodha
Hesabu ni orodha ya seva ambazo Ansible itadhibiti kiotomatiki kupitia kitabu cha kucheza.
[snowflake]
ip-address
5. Peleka/ Sambaza
Mwishowe, kwa kuendesha playbook, Ansible itapeleka proksi inayojitegemea Snowflake.
Unaweza kuiendesha kama root:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u root
Au na sudo:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u username -b
6. Dhibiti proksi ya Snowflake
Ikiwa mwenyeji wa proksi ya Snowflake inaendesha systemd, unaweza kudhibiti proksi yako ya Snowflake kwa kutumia amri za systemd: kuanza, hali na kuacha.
Kwa mfano:
$ ansible all -i inventory -a 'systemctl status snowflake-proxy'
Kwa FreeBSD, unaweza kudhibiti proksi yako ya Snowflake kwa kutumia amri hizi za maandishi ya rc.
Kwa mfano:
$ ansible all -i inventory -a 'service snowflake status'
7. Kuboresha proksi yako ya Snowflake
Ni muhimu kuweka proksi yako ya Snowfake inayojitegemea iwe imesasishwa.
Kuendesha playbook ya Ansible kutasakinisha masasisho:
$ ansible-playbook -i inventory site.yml -u root
8. (Si lazima) Kupunguza matumizi
Unaweza punguza idadi ya wateja (watumiaji wa Snowflake) kw kutumia client.
Upeo wa juu wa wateja wanaotumia wakati mmoja kwa chaguo-msingi hauna kikomo (0 = isiyo na kikomo).
Playbook iliyopo hapa chini ina kikomo 300 ya wateja wanaotumia wakati mmoja:
- hosts: snowflake
vars:
clients: 300
roles:
- nvjacobo.snowflake
Kumbuka Kigezo hiki cha jukumu la Ansible kinachofaa hakipatikani kwa FreeBSD.